
MWANAFUNZI wa darasa la 7 shule ya msingi Mwenge manispaa ya Morogoro, Faidhati Ibrahim (13), ameuawa kwa kukatwa na mapanga na binamu yake Shomari Malima, akiwa nyumbani kwao mtaa wa Tambukareli, huku sababu ikitajwa ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama wa marehemu na mama wa mtuhumiwa.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tambukareli, Kata ya Kingolwila Juma Muitano, amesema tukio hilo limetokea jana Februari 15, 2022, majira ya saa 12:30 jioni ambapo baada ya kupata taarifa wakazi wa mtaa huo walianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa bila mafanikio na kuliachia jeshi la polisi kuendelea uchunguzi wake.