×

Wafungwa zaidi ya 100 wagoma kula

ZAIDI ya wafungwa 100 wa Sudan wakiwemo wanasiasa wa ngazi za juu, wameanza mgomo wa kula katika Gereza la Soban.

 

Kupitia taarifa kamati ya mawakili wanaowawakilisha waandamanaji wanaoshikiliwa kinyume cha sheria imesema zaidi ya wafungwa 100 katika gereza hilo wameanza mgomo wa chakula kufuatia kufungwa kwao kinyume cha sheria.

 

Wafungwa hao ni sehemu ya vuguvugu la maandamano ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ambayo yaliondoa utaratibu uliowekwa wa uongozi wa kugawana mamlaka kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2019 dhidi ya rais wa zamani Omar al-Bashir.

 

Kulingana na Kamati Kuu ya Madaktari wa Sudan Kufuatia mapinduzi ya Oktoba 25, watu 81 wameliuawa huku vifo vingi vikitokea katika majuma mawili yaliyopita na watu wengine 2000 kujeruhiwa.

Leave a Comment