×

Mapomoroko Yaua Watu 100

TAKIBANI watu 100 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi na mafuriko katika mji wa Petrópolis nchini Brazil, Jiji hilo, ambalo liko kwenye milima kaskazini mwa Rio de Janeiro, lilikumbwa na mvua kubwa.

 

Nyumba katika vitongoji vya milimani ziliharibiwa na magari kusombwa na maji huku mafuriko yakipita katika mitaa ya jiji hilo.

 

Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Brazil lilisema watu 24 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa, na zaidi ya vifo 94 vimethibitishwa.

Video zilizizosambaa  kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha uharibifu mkubwa na magari yakielea mitaani.

Leave a Comment