×

Chico Yamkuta, Aondolewa Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Chico Ushindi, atakaukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kutokana na kuumwa ghafla.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Februari 25, mwaka huu mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa
Manungu, Turiani mkoani
Morogoro.


Akizungumza na Spoti
Xtra, Daktari wa Viungo wa Yanga, Mtunisia, Youssef Ammar, alisema kiungo huyo alipata maumivu ya misuli siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Biashara United uliochezwa juzi Jumanne.


Ammar alisema Chico
alikuwepo katika mipango ya kucheza mechi hiyo ya juzi, lakini maumivu aliyoyapata yalisababisha aondolewe kikosini.

“Chico alikuwepo katika mipango ya kocha kuanza kikosi cha kwanza dhidi ya Biashara, lakini alikuja kuondolewa saa chachebaada ya kupata maumivu ya misuli akiwa mazoezini.


“Kuondolewa kwake
kuliharibu mipango ya kocha, hivyo kutokana na maumivu hayo aliyoyapata, atatakiwa kukaa nje ya uwanja kuanzia siku saba hadi kumi kwa ajili ya kupatiwa matibabu, hivyo huenda akaukosa mchezo ujao wa ligi dhidi ya MtibwaSugar,” alisema Ammar.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

“MSINIPE POLE” – LUKUVI AZUNGUMZA AKIMKABIDHI OFISI WAZIRI ANGELINA MABULA..

Leave a Comment