
BINGWA mara saba wa mbio za Formula 1, Lewis Hamiliton amethibitisha kuendelea kukimbiza magari kwenye mbio hizo za Langa langa msimu huu wa 2022 amesema hajawahi kutangaza kustaafu, dereva huyo wa Mercedes amesema hayo wakati wa uzinduzi wa magari mapya watakayotumia msimu huu.
Hamilton ameongea na vyombo habari kwa mara ya kwanza tangu alipoukosa ubingwa wa Formula One, msimu uliopita mbele ya Max Verstappen wa Red Bull, kwenye mzunguko wa mwisho kwenye mbio za Abu Dhabi mwezi Novemba mwaka jana.
“Sijawahi kusema nitaacha, ninapenda kufanya ninachofanya, ni fursa kwangu, unajisikia kama familia hakuna hisia kama hii, ulikuwa wakati mgumu kwangu, nilihitaji kupumzika kidogo, nikizingatia zaidi wakati huu, na familia yangu na kuwa na wakati mzuri.” Amesema Hamilton
Hayo yamejiri ikiwa ni siku moja tu imepita tanga uongozi wa Formula One ulipotangaza kumuondoa Michael Masi kama Mkurugenzi wa kuongoza magari ya Langa langa (Race Director).