×

Kauli ya Nape Kuhusu Bunge Live

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema serikali inaliangalia suala la kurejesha Bunge Live ili wananchi waweze kutazama na kusikiliza mijadala inayoendelea bungeni.

 

Nape amesema hayo leo Jumatatu, Februari 21, 2022 wakati akihojiwa katika Kipindi cha 360 cha Clouds TV.

 

“Kuhusu Bunge Live, Spika Dkt. Tulia Ackson alisema hili jambo linazungumzika na tutajadiliana na serikali tuone namna ya kulifanya liende.

 

“Studio ya Bunge ndiyo inaamua warushe vipi matangazo, najua kwa mfano Afrika Kusini wana-delay fulani yaani kwamba wanarusha live bunge lakini kuna delay ya dakika 15 au nusu saa, hako ka-delay kanawapa room wabunge waone kama katafaa kwenda hewani.

 

“Kwa mfano ikatokea wabunge wanarushiana maneno machafu bungeni (hatuombei) na tumeona baadhi ya mabunge ya wenzetu wanapigana sasa vitu kama vile havipeleki sura nzuri.

 

“Kupeleka dakika 15 au nusu saa sio mbaya lakini isipitilize na kuwe na utaratibu kwamba kama kuna jambo fulani la kujadili na wabunge wakaona linafaa tu kujadiliwa ndani, suluhisho ni kanuni ya kuendesha studio ya bunge ambayo ni kazi ya bunge,” amesema Nape.

 

Leave a Comment