×

Arteta Ampa Tano Pepe

BOSI wa Arsenal, Mikel Arteta, amefunguka kuwa, nyota wake Nicolas Pepe amebadilika na anaamini atakuwa mchezaji muhimu kikosini katika kusaka nafasi ya kumaliza ligi ndani ya nne boramsimu huu.


Pepe msimu uliopita wa
2020-21, alikuwa akitokea sana benchi ambapo alifanikiwa kufunga mabao sita katika Premier.

Msimu huu hajaanza vema akiwa amefunga mabao mawili.Wakati akishindwa kufanya vizuri na Arsenal, hivi karibuni akiwa na Timu ya Taifa ya Ivory Coast kwenye michuano ya AFCON 2021, alionesha kiwango bora, licha ya timu yake kushindwa kufika mbali zaidi, lakini aliondoka na mabao mawili akicheza mechi nne.


“Pepe kwa sasa
amebadilika, uwanjani ana tabasamu, ana nguvu mpya na amekuwa na mawasiliano na kila mmoja, mazoezini yupo vizuri, anaonesha ni mchezaji muhimu ndani ya timu.


“Tangu ametoka katika
michuano ya AFCON, nafikiri Nico amebadilika kwa kiasi kikubwa sio kama awali. Sijui nini kimetokea, amekuwa na msimu mzuri, ninaamini atakuwa na mchango mkubwa hasa tukiwa
mwishoni mwa msimu.


“Kama timu tunamuhitaji
kwa sababu kila mchezaji lazima atoe mchango wake, ukiangalia kwa sasa kikosi chetu sio kipana. Sipendi kuona mchezaji anakaa sana benchi ndiyo maana nimeamua kumpa nafasi kuonesha uwezo,” alisema Arteta.

Leave a Comment