×

Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Tanzania PLC Azuru Vyombo vya Habari

Mwenyekiti wa Clouds Media Group Joseph Kusaga (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kuhusu mipango-mkakati ya Vodacom kwa mwaka huu wa 2022 wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea ofisi za Clouds Media na kupata fursa ya kujitambulisha kwa wafanyakazi chombo hicho. 

 

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu (kushoto) Mkurugenzi huyo alipotembelea kwenye za Mwananchi na kupata fursa ya kujitambulisha kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC , Rosalynn Mworia.

 

 

Meneja Matangazo EATV, Lidya Igarabuza (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kuhusu mipango-mkakati ya Vodacom kwa mwaka huu wa 2022 wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo mpya wa Vodacom kutembelea ofisi za IPP Media ambapo EATV/Radio ni mojawapo.

 

 

Mhariri Mkuu wa Gazeti la The Guardian, Wallace Maugo (kulia) akielezea namna ya uendeshaji wa kila siku wa gazeti hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC , Rosalynn Mworia (kushoto).

 

 

 

Mwenyekiti wa Clouds Media Group Joseph Kusaga (katikati) akimkaribisha Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kwenye kipindi cha XXL Clouds Fm kinachoongozwa na Adam Mchomvu (kulia).

Leave a Comment