×

Nabi Awabadilishia Mbinu Mtibwa Manungu

MECHI ya kisasi! Ndivyo utakavyosema katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaozikutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga utakaopigwa leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.


Timu hizo zitavaana katika
mchezo wa kwanza wa ligi, lakini Mtibwa wataingia uwanjani wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa katikamchezo wa mwisho msimu uliopita bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Angola, Fernandos Carinhos.


Wakati Mtibwa wakiingia
kutaka kulipa kisasi, Yanga wenyewe wanahitaji pointi  tatu ili waendelee kukaa kileleni kwa kuwaacha watani wake kwa gepu kubwa la pointi katika msimamo wa ligi.


Yanga inaongoza katika
msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 ikifuatiwa na watani wao Simba wenye 31 huku
Mtibwa 12 wakiwa katika
nafasi ya 14.


Akizungumzia mchezo
huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi alisema kuwa anafahamu
anakwenda kucheza
mchezo mgumu dhidi ya Mtibwa huku akiwa amekiandaa kikosi chake kukabiliana na changamoto zote watakazokutana nazo.

 

Nabi alisema kuwa moja ya changamoto anayokwenda kukutana nayo ni ubovu wa uwanja, ambao kwake
hataki iwe sababu ya
kupoteza mchezo huo muhimu kwao kupata matokeo mazuri.


Alisema kuwa siku tatu
alizotumia kukiandaa kikosi chake kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam,
zimetosha vijana wake
kupata matokeo mazuri, licha ya changamoto ya uwanja watakayokutana
nayo.


“Nimeki
andaa kikosi changu kutokana na aina ya uwanja  nitakaokwenda kuutumia dhidi ya Mtibwa, siufahamu lakini nimepata taarifa za uwanja huo.


“Mimi
ninakiandaa kikosi changu katika mazingira yote, kwani uzuri nafahamu changamoto iliyopo hapa nchini ya viwanja,uzuri vijana wangu wanafahamu vizuri hivyo sina hofu, tumejiandaa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, licha ya kukabiliwa na majeraha kikosini kwangu,”alisema Nabi.

 


Kwa upande wa Kocha
Msaidizi wa Mtibwa, Awadh Juma, alisema: “Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri.


“Tunashukuru namba
ya wachezaji waliokuwa wana majeraha imepungua, tunaamini kwetu yatakuwa mazingira rafiki kutokana na kutumia uwanja wa nyumbani.

 

“Morali ipo juu kwa wachezaji wetu wote, hivi sasa tunawatengeneza kisaikolojia tu kutokana na ukubwa
wa mchezo huu,
kwani mazoezi ni yaleyale wanayofanya kila siku,” alisema Juma.

STORI: WILBERT MOLANDI, DAR ES SALAAM

Leave a Comment