
BINTI wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Dkt. Angela Nagasha Kakishozi amemtambulisha rasmi mpenzi wake wa muda mrefu, Amanya Tumukunde ambapo wanatarajiwa kufunga ndoa Jumamosi, Februari 26 katika Kanisa la St Paul’s Cathedral, Namirembe, Kampala, Uganda.
Mchumba wa Angela ni mtoto wa Jenerali Henry Tumukunde, aliyekuwa mgombea urais wa nchi hiyo. Angela na Amanya ambao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu tangu utotoni, na walisoma pamoja nchini Malaysia, wamefanya harusi ya kitamaduni Jumamosi iliyopita, Februari 19, 2022.
Sherehe hiyo ya faragha ilihudhuriwa na jamaa na marafiki wachache wa karibu.