Global TV imefanya mazungumzo na Mariam, mama ambaye aliyeacha kazi ya mama lishe na kugeukia kazi ya udereva wa malori ya mizigo yanayofanya safari nje za nchi. Mariam ametupitisha kwenye historia yake huku akieleza mikasa mizito aliyowahi kukutana nayo akiwa safarini ikiwemo kushuhudia madereva wenzake wa malori wakiuawa nchini Congo.