×

Sakho, Banda Wampa Jeuri Pablo Simba

VIWANGO bora vinavyoonyeshwa na mawinga wa Simba, Pape Ousmane Sakho na Peter Banda vinampa jeuri kocha wa timu hiyo, Pablo Franco kuelekea mchezo wao dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Pablo ameliambia Championi Jumamosi, kuwa viwango vya wachezaji hao vimezidi kuimarika baada ya kuanza vibaya ndani ya timu hiyo kutokana na sababu mbalimbali.

 

“Timu kwa ujumla imeimarika, hali ambayo ipo kwa sasa ni tofauti na ya kipekee sana kwani ukitazama ni tofauti na ilivyokuwa huko mwanzo. Kuna wachezaji wengi walikuwa wakipitia katika wakati mgumu lakini kwa sasa ni tegemeo kwenye kikosi.

 

“Banda, Sakho wote walipitia wakati mgumu hapo mwanzo lakini kwa sasa kila kitu kipo tofauti na ni tegemezi katika timu. Wameimarika sana na wana mchango mkubwa na wataendelea kutusaidia katika michezo yetu ijayo haswa hii ya kimataifa kutokana na uwezo wao,” alisema kocha huyo.

Stori: Marco Mzumbe

Leave a Comment