×

Yanga vs Kagera; Vita ya Kisasi Kwa Mkapa Leo

LEO Uwanja wa Mkapa uliopo Temeke, Dar es Salaam, itakuwa ni vita ya kisasi kwa Yanga inayonolewa na
Nasreddine Nabi dhidi ya
Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza, ukiwa ni mchezo wa
Ligi Kuu Bara.

 


Yanga ni vinara katika
Ligi Kuu Bara, mchezo wa kwanza walishinda bao 0-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba,
Kagera na mtupiaji alikuwa
ni Feisal Salum, ambaye leo ataukosa mchezo kutokana na
kutumikia adhabu ya kadi tatu
za njano.

 


Akizungumza na Spoti Xtra,
Baraza raia Kenya, alisema wanatambua Yanga ni timu imara na haijapoteza mchezo
msimu huu, hivyo wataingia
kwa tahadhari katika kujilinda na kushambulia.


“Mchezo wetu na Yanga
utakuwa mgumu, lakini timu itakayoweza kumiliki eneo la kati ina nafasi kubwa ya kushinda. Kucheza mechi 15 bila kufungwa hilo ni jambo kubwa,” alisema Baraza.

 

Nabi alisema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila amewaambia wachezaji wake wacheze kwa
juhudi.

“Nimewaambia wachezaji wacheze kwa kujituma, nitakosa huduma ya Dickson Job ambaye ana adhabu,
Chico Ushindi huyu alikuwa
nje kwa muda kutokana na majeraha, hivyo anaweza kuanza ama kutokuanza kwa
kuwa bado hajawa fiti, Yassin
Mustapha yupo safi, Kibwana Shomari hatacheza pia,” alisema Nabi.


Nyota wa Kagera Sugar,
Hamisi Kiiza, alisema akipata nafasi atafunga ama atatoa pasi ya bao, lakini hataki
kupata kadi katika mchezo
huo.


“Ikiwa nitapata nafasi
nitafunga ama kutoa pasi ya bao, lakini sitaki kupata kadi ya njano ama nyekundu kwenye mchezo wetu,” alisema Kiza ambaye aliwafunga Simba walipocheza Kaitaba.

STORI; LUNYAMADZO MLYUKA NA MARCO MZUMBE

NDEGE YA ZANZIBAR YADONDOKA BAHARINI COMORO, MARUBANI 2 WA TANZANIA HAWAJULIKANI WALIPO..

Leave a Comment