×

Unachopaswa Kufanya Ili Mume Asichepuke

RAFIKI,mapenzi yana kanuni zake; kanuni ambazo usipozifuata huwezi kupata furaha uliyotarajia. Unapotokea
kumpenda mtu, hiyo ni hatua ya kwanza,
lakini omba sana upate ile bahati ya kumpenda mtu ambaye naye anakupenda kwa dhati.


Kwa bahati mbaya ukitokea kumzimikia mtu
ambaye wala hana hata chembe za penzi kwako, utaumia sana na kama utalazimisha kuwa naye, utakuwa unajitafutia vidonda vya tumbo.

 

Hata hivyo, wapo waliobahatika kuwapata wapenzi wa ukweli, lakini kwa kushindwa kwao kujua yapi ya kufanya ili kudumisha penzi, leo hii wameachika na bado wanaranda mtaani.

 

Kwa kifupi ni kwamba, unapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu na ukabaini naye anakupenda, hutakiwi kubweteka, bali unatakiwa kutumia utundu na ubunifu wako katika yale ambayo yatamfanya huyo mtu wako ahisi wewe ni wa pekee kwake.


Ninapozungumzia hayo, namaanisha ubunifu
kwenye mambo mengi ambayo hakika nikianza kuyaelezea hapa, nafasi inaweza isitoshe ila kwa leo nigusie utundu katika uwanja wetu ule wa kujidai.


Faragha ni eneo muhimu sana ambalo
linaweza kubomoa au kuimarisha ndoa. Ninapozungumzia hilo, ni kwa wote; yaani mke na mume.


Mwanaume anatakiwa kumridhisha mkewe
kwa kiwango kinachostahili. Kusiwepo mazingira ya kupeana mambo kiduchu kwani ikiwa hivyo lazima mke atakosa furaha iliyokamilika. Ila sasa leo nataka niwazungumzie kwa
kirefu wanawake.

 

Kuna wanawake ambao wamebahatika kupata wanaume au waume wanaowapenda sana na kuwapatia kila wanachohitaji.


Hawa wanatakiwa kujiona ni wenye bahati
kubwa kwani kwa hali ilivyo sasa, wanawake wengi wanatafuta wanaume wa kuwaoa hawawapati.


Kinachonishangaza ni kwamba, kuna baadhi
ya wanawake ambao wako ndani ya ndoa, lakini  wamejisahau kwamba wana jukumu la kuwapa waume zao furaha ambazo hawawezi kuzipata kwingine.


Ukijaribu kuchunguza utabaini wanawake
wengi walio ndani ya ndoa siku hizi wanasalitiwa sana. Hii ni kwa sababu wamekuwa waongeaji sana, lakini wanapokuwa faragha unaweza ukadhani siyo wao. Hawajui kitu, wamekaa kama
magogo tu halafu eti wanadhani hawatasalitiwa
na ndoa zao zitadumu, zitadumu kwa misingi ipi?


Mwanamke akae akijua kwamba, mumewe ni
kama mtoto ambaye anatakiwa kubembelezwa huku akipewa vitu vitamu ili kumpumbaza asishawishike kutoka nje. Ukiwa kwenye ndoa kisha ukachukulia kila kitu poa tu eti kwa kuwa tayari ulishapendwa ipo siku utajikuta ni mke wa pambo la nyumba tu.


Mtaani kuna utitiri wa nyumba ndogo,
wanaume walioanzisha makoloni hayo nje ya ndoa zao walikosa wake sahihi ambao wanaweza kuwashikilia waume zao.

Matokeo yake sasa nyumba ndogo hizo ndizo zinazooonekana kuwashika waume za watu siku hizi na wanafanikiwa kwa kuwa ni watundu na wabunifu.


Sasa kwa nini wewe mwanamke uliye ndani ya
ndoa usifanye kama yale wanayofanya nyumba ndogo? Kuna dada mmoja nilizungumza naye hivi karibuni akaniambia eti amenuniana na mumewe huu ni mwezi wa pili baada ya mwanaume wake huyo kutaka afanyiwe mambo ambayo yeye aliona kinyaa kuyafanya.


Kabla ya kumjibu kwanza niliguna, sababu ya
kuguna ni kwamba niliyagundua hayo mambo ambayo aliona kinyaa kumfanyia mumewe.

Niseme tu kwamba, mapenzi wakati mwingine ni uchafu, wanaojua mapenzi wanajua kwa nini nasema
hivyo.


Nilichomjibu mwanamke huyo ni
kwamba, kama mwanaume huyo anampenda amfanyie kila atakacho isipokuwa kukubali kufanya mapenzi kinyume na maumbile na nikamwambia kuwa, mapenzi ni uchafu hivyo hayo ambayo anaona kinyaa kumfanyia mumewe ndiyo ambayo wengine wamekuwa wakiyafanya na wamefanikiwa kuzishika ndoa zao.


Naomba niseme tu kwamba,
huenda unajiamini kuwa ni mzuri na umbo la kuvutia kiasi kwamba, ni rahisi kupata mwanaume wa kuoa lakini tambua bado utakuwa na kazi kwenye kuidumisha ndoa na kuhakikisha hukaribishi mazingira ya mumeo kutafuta nyumba ndogo.

Hakikisha unaonesha uanamke wako ili hata kama huyo mumeo atatoka nje, iwe ni kwa tamaa zake tu lakini mambo ya msingi uwe unampatilizia.Kwa leo naomba kuishia hapa, tukutane JUMATATU ijayo. Kwa maoni na ushauri, wasiliana name kwa WhatsApp namba; 0713 750 910.

 

Leave a Comment