×

Kodak Black: Wanaume Hawatakiwi Kuoga Kila Siku

Rapa maarufu nchini Mmarekani, Bill Kahan Kapri almaarufu Kodak Black, amesema kuwa wanaume hawastahili kuoga kila siku na kwamba wanaume na wanawake wana viwango tofauti ikifikia suala la usafi wa mwili.

Kodak ameyasema hayo katika mahojiano na Atlanta’s 105.3 The Beat, baada ya mwendeshaji wa shoo hiyo Jo Jo Alonso kulalamika kuwa wanaume wengi hawachukulii usafi wao kwa uzito na wananuka.

Akimjibu Alonso, msanii huyo aliyevuma na wimbo wa  Super Gremlin, amesema kuwa sio lazima wanaume waoge kila siku tofauti na mwanamke ambaye lazima aoge mara nyingi kwa siku.

Leave a Comment