
Nahreel; ni producer na msanii wa Kundi la Navy Kezo linaloundwa na yeye na baby mama wake, Aika na kwa pamoja wanamiliki lebo ya muziki ya The Industry.
Katika hali inayoibua sintofahamu, Nahreel ameibuka na kukanusha tetesi kwamba ana mtoto nje ya uhusiano wake na Aika.
Nahreel ameandika; “Habari za mimi kuwa na mtoto nje zimekuwa ni nyingi na ni za uongo, naomba muheshimu familia yangu.
“Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blogs mbalimbali na watu mbalimbali maarufu pia wamekuwa wakiposti bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari siyo za kweli.
“Nina watoto wawili @gold_navykenzo na @jamaika_navykenzo. Na nimezaa na mwanamke mmoja @aikanavykenzo Kuweni makini mnapotoa habari familia yetu haiendekezi umbeya ila hii imevuka mipaka…
Nahreel na Aika imekuwa ni kapo ya mfano kwa kuwa wamedumu kwa muda mrefu bila kokoro, lakini inavyoonekana kuna wanga wanataka kuharibu mambo.