
RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa mataifa ya Magharibi kuimarisha vikwazo dhidi ya Urusi, akikosoa viongozi kwa kutojibu tangazo la awali la Wizara ya Ulinzi ya Urusi kuhusu kushambulia majengo ya kijeshi na viwanda ya Ukraine.
Pia, Zelensky ametoa wito wa kuwafikisha mahakamani wanaoamuru na kutekeleza uhalifu huo akisema hawajali na wanatangaza wazi ukatili uliopangwa kufanyika.
Ameeleza kuwa, ujasiri huo ni ishara tosha kwa nchi za Magharibi kwamba vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi havitoshi.