×

Harmonize Matatani Kupanda Stejini na Mtoto

STAA wa muziki na CEO wa Konde Gang, Harmonize amejikuta pabaya mara baada ya kukosolewa vikali na wadau mbalimbali wanaosimamia haki za watoto nchini kufuatia kitendo chake cha kupanda stejin usiku na mtoto wake wa kike Zuuh Konde katika tamasha lake la Afro East Carnival lilifanyika wekeend iliyopita katika Uwanja wa Tabata Shule jijini Dar es salaam.

Kupitia kipindi cha Leo Tena ya Clouds FM, wamethibitisha kuwa msanii huyo kwa sasa anasakwa na mamlaka za Ustawi wa Jamii wilaya ya kinondoni, kufuatia kitendo chake hicho cha kuambatana na kumpandisha mtoto mdogo katika tamasha lililo fanyika usiku mkubwa.

Leave a Comment