Rais Samia Akutana na Wake wa Viongozi Ikulu, Zanzibar
Global Publishers March 9, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na wake wa viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar Machi 8, 2022 Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Rais Samia Suluhu Hassan leo Machi 8, 2022 amekutana na wake wa viongozi mbalimbali wa Serikali Ikulu Tunguu, Zanzibar mara baada ya kuzungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Rais Samia akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Wake wa Viongozi mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022.Rais Samia akipokea zawadi ya picha kutoka kwa mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar.Rais Samia akiwa katika picha ya kumbukumbu na mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi mara baada ya hafla hiyo fupi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 08 Machi,2022.Rais Samia akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mke wa Makamu wa Rais Mbonimpaye Mpango, Mke wa Rais wa Zanzibar Mariam Mwinyi pamoja na Wake wa viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022.