
SHILOLE au Shishi Baby; ni mwanamama anayefanya Bongo Fleva na ni mjasiriamali ambaye amefunguka kuhusu kumsukuma ndani (polisi) mmoja wa ma-X- wake kwa kuposti picha zao za zamani.
Shishi amefunguka hilo wakati akijibu swali kwenye Kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM;
“Sipendi ambacho ma-ex wangu wanakifanya hasa mmoja ambaye yeye anaposti picha za zamani na nimeshampeleka mpaka polisi na akasema hatarudia, lakini bado anafanya.
“Mimi nikiwa kwenye uhusiano huwa nafanya mema na ndiyo maana unaona wengi wananizungumzia kwa mazuri kwa sababu huwa natenda mema,” anasema Shishi ambaye ma-X wake wanaofahamika ni Nuh Mziwanda na Uchebe
sifaelpaul