
Usiku wa kuamkia leo Ijumaa Machi 11, 2022, Diamond Platnumz ameachia albam fupi (EP) yake ya First Of All (FOA) yenye jumla ya nyimbo 10.
Uzinduzi umefanyika pale Slipway jijini Dar na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali wakiwemo mastaa wa ndani na nje ya Bongo.
Tofauti na EP zote zilizotolewa na wasanii mbalimbali nchini Tanzania, EP ya Diamond ndiyo yenye nyimbo nyingi zaidi ambazo zipo kumi.
Diamond mwenyewe anasema kuwa, nyimbo zipo nyingi na yeye na uongozi wake walipata wakati mgumu mno wa kuchagua ni nyimbo gani ziingie humo huku nyingine zikisubiria albam itakayotoka baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa wahudhuriaji ambao wamepata fursa ya kusikiliza nyimbo zote wamekiri kwamba EP ya Diamond ni ya moto mno huku wakitofautiana nyimbo wanazozikubali.
Nyimbo hizo na walioshikishwa na Diamond ni kama zifuatavyo;
Melody –Diamond FT Jaywillz
Somebody –Diamond
Fine –Diamond
Mtasubiri –Diamond FT Zuchu
Sona –Diamond FT Adekule Gold
Loyal –Diamond
Wonder –Diamond
Nawaza –Diamond
Oka –Diamond FT Mbosso
Fresh –Diamond FT Focolistic & Costa Ticht & Pabi Cooper.
