Kumekuwa na ripoti za milipuko katika miji ya pande tofauti za nchi katika muda wa nusu saa iliyopita.
Vyombo vya habari vimearipoti milipuko huko Lutsk Kaskazini-Magharibi, na vile vile huko Dnipro – jiji la bara lililoko kwenye mto Dnieper na ngome kuu katikati mwa mashariki mwa Ukraine.

Picha za satelaiti za msafara wa Urusi karibu na Kyiv zinaonekana kuonyesha vikosi vikitumwa tena katika maeneo ya karibu, na hivyo kuashiria msukumo mpya kuelekea mji mkuu wa Ukraine.
Kulingana na Maxar Technologies, sehemu ya msafara huo – ambao ulionekana mara ya mwisho kaskazini-magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Antonov ulio karibu – umehamia katika miji inayozunguka.
Maxar ilisema kuwa picha zinaonyesha sehemu zingine za msafara wa kaskazini zimejipanga karibu na Lubyanka, na kuweka sehemu za mizinga karibu.
Mapema siku ya Alhamisi, afisa mkuu wa ulinzi wa Marekani alisema kuwa vikosi vya Urusi vimesogea maili tatu (5km) karibu na Kyiv katika muda wa saa 24 zilizopita.