
KATIKA kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kitengo cha walimu wanawake mkoa wa Kilimanjaro kimeadhimisha siku hiyo kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum.
Akizungumza na mwandishi wetu mmoa wa walimu wa kitengo hicho aliesema;
“Katika shule ya Msandaka Lions Deaf Center iliyopo Manispaa ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro shule hii ina watoto ambao hawana uwezo wa kusikia na baadhi ambao hawana uwezo wa kuona vizuri.

“Shule hii inakabiliwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu wenye taaluma ya kufundisha watoto hao lakini pia barabara kuharibika hasa kipindi cha mvua.
“Ni kwa muda mrefu sasa shule hii ya kiserikali imekuwa ikitegemea sana msaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali kwani wanafunzi huishi bweni na hivyo mahitaji ya watoto wanaosoma shule hii kama chakula, madaftari ,kalamu na mengineyo kuwa makubwa kulingana na pesa wanayoipata kutoka serikalini.
“Kutokana na changamoto hizo na nyingine ndizo ambazo hugusa jamii inayowazunguka kuwakimbilia kwa hali na mali.
“Kadhalika kupelekea chama hicho kuwakumbuka kwa kushiriki kukaa nao pamoja lakini pia kuwapatia mahitaji ambayo kwa namna moja au nyingine yanayoweza kuwafariji na kuwatoa katika upweke na wao kutambua wapo wanaowajali” alisema mwalimu huyo.
Wito kwa walimu hao na walimu wa shule zingine kwa ujumla ni kutambua kwamba jamii inawakumbuka watoto hao na wazidi kufarijika na mwisho kutimiza malengo yao. HABARI/PICHA NA ISAACK MAKOI /GPL KILIMANJARO