
HIFADHI ya taifa ya Kilimanjaro imepokea jumla ya wageni 28 raia wa Marekani ambao walipanda mlima Kilimanjaro tar.04.03.2022 kupitia lango la Lemosho kati ya wageni hao miongoni mwao takribani wageni 22 kutokea Marekani walichangia figo kwa watu mbalimbali.
Akizungumza baada ya kumaliza kupanda mlima huo wakiwa katika lango la kutokea aliyekuwa akiwaongoza watalii hao alisema;

“Na leo tupo katika lango la mweka ambapo wageni hao walichukua takribani siku 8 kufika tar.11.3.2022 kwa mwendo wa polepole kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro chenye urefu wa zaidi ya kilometa 5000 ambao ni mlima pekee mrefu Barani Africa na pia mlima mrefu duniani uliosimama peke yake kwa hakika.
“Huu ni ushujaa wakipekee kwa wageni hawa wakiidhirishia dunia kuwa kuchangia figo si mwisho wa maisha bado kunauwezekano mkubwa wakuendelea na shughuli zako za kila siku katika jamii inayokuzunguka.
“Tumepata wasaa wakuwasililiza wageni hawa lakini pia uongozi wa hifadhi hii wametuambia neno hapa kwamba licha tu ya kupanda na kutangaza mlima Kilimanjaro lakin lengo lao lakupanda mlima huu pia ilikuwa ni kuikumbusha jamii juu ya kuwasaidia wagonjwa wa figo” alimaliza kusema muongoza watalii hao.
HABARI/PICHA NA ISAACK MAKOI /GPL.