×

Bodi ya Wakurugenzi TRA Yavutiwa na Uwekezaji wa SBL

Mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa Kampuni ya Bia ya SBL John Wanyancha (kushoto) akiongea na wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) muda mfupi kabla ya ziara ya kutembelea kiwanda cha SBL Dar es Salaam kuangalia namna mfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanyakazi katika kiwanda hicho jana.

 

 

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Serengeti (SBL) cha Dar es Salaam na kuelezea kuridhishwa na uwekezaji inayofanya kampuni hiyo hapa nchini.

Wajumbe wa wa bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na mwenyekiti wao Mussa Ulledi wakielekea kwenye sehemu ya kufungashia (packagingarea) kwaajli ya kukagua utekelezaji wa mfumo wa stempu za kielekroniki katika kiwanda cha kampuni ya bia ya Serengeti kilichopo Dar es Salaam.

 

 

Akiongea katika ziara hiyo iliyolenga kuangalia namna zoezi la utekelezaji wa stempu za kielekroniki unavyoendelea, mwenyekiti wa bodi hiyo, Ulledi Mussa alisema uwekezaji unafanywa na SBL una tija kubwa kwa taifa.

Meneja ufungashaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti Praygod Minja akimwelekeza Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata namna mfumo wa stempu za kielekroniki unavyofanyakazi alipotembelea kiwanda hicho jana pamoja na wajumbe wa bodi ya TRA. Nyuma yao ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti.

 

 

“Upanuzi mkubwa wa viwanda vyenu unaonyesha kuwa mpo na mtanendelea kuwepo. Serikali ipo nyuma yenu na changamoto mbalimbali za kikodi zitakuwa zikiendelea kufanyiwa kazi ili kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya kufanya biashara zenu,” alisema.

 

Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa TRA inaichukulia kampuni ya SBL kama mdau muhimu wa maendeleo na kushukuru kwa uwekezaji wake katika miradi mbalimbali ya kijamii.

 

Kwa upande wake, mkurugenzi wa mahusiano kwa umma wa SBL John Wanyancha alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwekeza katika miradi mbalimbali ya kijamii kama vile maji, elimu, kilimo endelevu na mingineyo.

Leave a Comment