×

‘Steve Nyerere Baiskeli Hajui Ndege Ataweza’

TUANZE mjadala polepole! Hivi tangu uzaliwe umeshawahi kusikia msanii Steve Nyerere akipiga gita au kurekodi singo ya muziki?

 

Umewahi kumsikia akiimba Taarabu labda? Umewahi kumsikia msanii huyu akipiga na kucheza ngoma za asili?

Umewahi kusikia akiimba kwaya kanisani, kaswida au hata zile za shule ya msingi na kugani mashairi?

Umewahi kumsikia Steve Nyerere akisajiliwa na bendi yoyote ya muziki wa dansi kuwa mpiga chombo chochote au mnenguaji jukwaani?

 

Kwa kumbukumbu zangu mbali na uingizaji wa filamu sijawahi kumuona au kumsikia akifanya hayo niliyoyataja; sijui wewe!

Lakini habari ya mjini ni kwamba, ameteuliwa kuwa msemaji wa wanamuziki wote nchini akiwemo Mzee Zahir Zorro.

 

Vigezo vilivyotumika kupitisha jina la Steve Nyerere; aulizwe msanii Fid Q ambaye ndiye katibu mkuu wa chama cha wanamuziki.

 

Baadhi ya wasanii wakongwe wameshapinga uteuzi huo; wanachomuuliza @stevenyerere2 ni hiki:
Baskeli hujui kuendesha helkopta utaendeshaje…?

Baadhi ya wasanii waliomtosa msanii huyo kwenye kina kirefu cha maji ni: “Nay Wa Mitego, Diamond, Wakazi, Adam Mchomvu, Q Chief, Afande Sele.”

 

Bila upendeleo wewe maoni yako ni yapi, @stevenyerere2 anafaa kushika nafasi hiyo au hafai? Karibu!

STORI NA MANYOTA | GPL

Leave a Comment