
ZUBERI Mohammed almaarufu Niva au Super Marioo; ni mwigizaji mkali wa kiume kunako Bongo Movies ambaye anasema kuwa, anachukizwa na jinsi watu wanavyomuita marioo (mwanaume anayelelewa na mwanamke) wakati hayuko hivyo.
Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Niva Anasema kwamba, aliamua kujiita jina la Marioo kwa sababu zake binafsi, lakini haikuwa na maana kwamba yeye ana tabia hizo za kimarioo hivyo ili kuepukana na kahfa hizo ndiyo maana ameamua kubadilisha jina hilo na kuamua kujiita Mr Kipenyo.
“Mwanzo nilijiita Niva Super Marioo kwa sababu zangu binafsi, lakini haina maana kwamba mimi ni marioo kweli, nachukia sana jinsi watu wanavyoniita jina hilo na kuwa dhana kwamba kweli mimi nina tabia hizo wakati siyo kweli ndio maana mwaka jana nilimua kuanza kujiita Mr Kipenyo ili kuepuka kashfa hizo na naomba muwe mnaniita hivyo,” anasema Niva aliyepata umaarufu wakati wa Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu.