
Kimeumana! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wasanii wa muziki Tanzania kukusanyika kwa ajili ya sintofahamu juu ya muigizaji Steve Nyerere kuwa msemaji wao.
Kwa niaba ya wasanii wa Dansi na Taarab, mwanamuziki Abdul Misambano amesema kuwa, kama ambavyo katika awamu ya nne Wizara ya Sanaa imetenganishwa na Wizara ya Habari, basi na wao wanaomba Bongo Fleva watafute msemaji wao huku Dansi na Taarab nao wawe na msemaji wao.
Mkutano huo unaendelea ndani ya Palm Village, Mikocheni jijini Dar.