
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo anatazamiwa kutangaza kwamba Uingereza itaipatia Ukraine takriban makombora 6,000 ya ziada.
Katika mikutano ya viongozi wa Nato na G7 mjini Brussels, Waziri Mkuu wa Uingeza Boris Johnson alitangaza ufadhili wa £25m kusaidia kulipa Wanajeshi na Marubani wa Ukraine.
“Uingereza itashirikiana na washirika wetu kuongeza uungaji mkono wa kijeshi na kiuchumi kwa Ukraine, kuimarisha ulinzi wao kadri wanavyobadilisha wimbi la vita hivi,” Johnson alisema.