
Coulibaly Ambaye Pia Anamudu Kucheza Beki Ya Kulia Na Kiungo Mkabaji, Mwenyewe Akizungumza Kutoka Ivory Coast Ameliambia Championi Jumatano Kuwa, Amekuwa Akisikia Kwa Watu Wake Wa Karibu Kuwa Simba Wanamfuatilia Wakitaka Kumsajili.
“Ni Kweli Simba Wanataka Kunisajili Lakini Mpaka Sasa Hawajanitafuta Wenyewe Rasmi Kusema Kuwa Wanataka Kunisajili Ila Ni Maneno Tu.
“Pamoja Na Hilo Haijalishi Kama Watakuwa Tayari Na Ofa Yao Itakuwa Nzuri Nitajiunga Nao,” Alisema Beki Huyo Mwenye Urefu Wa Futi 5 Na Inchi 10.