
Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) leo Mach 29, 2022 wameidhinisha rasmi ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za EAC ametangaza leo Machi 29 wakati wa Mkutano wa 19 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za EAC uliofanyika kwa njia ya mtandao.
