
Mwigizaji Will Smith amemuomba msamaha Chris Rock baada ya kumpiga kibao katika jukwaa la ugawaji wa Tuzo za Oscar akisema tabia yake haikubaliki na haina udhuru “Ningependa kukuomba msamaha hadharani, Chris, nilivuka mpaka na nilikosea”
Haya yanajiri baada ya Chuo cha filamu cha Oscars kilimlaani Smith juu ya tukio hilo na kutangaza kwamba inatathmini marekebisho rasmi, Smith alimpiga kibao Rock jukwaani baada ya Mchekeshaji huyo kufanya utani kuhusu Mke wa mwigizaji huyo, Jada Pinkett Smith.
Rock alimtania Jada Smith kwa kunyoa nywele, baaada ya kuzipoteza kutokana na hali inayofahamika kama alopecia, muda mfupi baadaye Smith alishinda tuzo yake ya kwanza ya Oscar kutokana na uigizaji wake kama Baba wa wachezaji nyota wa tennis Venus na Serena Williams katika filamu ya King Richard.
“Vurugu njia zote ni sumu na uharibifu, mwenendo wangu wa jana usiku katika Tuzo haukubailiki na hauna udhuru, utani ni sehemu ya kazi lakini mzaha kuhusu hali ya kiafya ya Jada ulikuwa mzito sana kwangu kuvumilia kihisia.”
Smith amemuomba msahamaha Rock moja kwa moja, akisema alivuka mpaka pia ameomba msamaha kwa Chuo na familia ya Williams “Ninajuta sana kwamba tabia yangu imetia doa safari ambayo imekuwa ya kupendeza kwetu sote”