×

Tigo Pesa na Axeva Wazindua Bahati Nasibu ya Dilipesa

Fabian Felician wa Tigo Pesa akizungumza kwenye uzinduzi huo.

 

 

KAMPUNI ya mtandao wa simu ya Tigo kupitia huduma yake ya Tigo Pesa kwa kushirikiana na Kampuni ya Axeva wamezindua mchezo wa kubahatisha uitwao Dilipesa ambapo washindi watakuwa wakiondoka na mkwanja kadiri watakavyokuwa wakicheza.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo mwakilishi wa kampuni ya Tigo Pesa, Fabian Felician amesema kampuni ya Tigo ambayo inaongoza kwa ubunifu na matumizi ya teknolojia ya kisasa imeanzisha mchezo huo ili kuwapa fursa wateja wake wanaotumia huduma ya Tigo Pesa kufanya miamala mbalimbali kuweza kujishindia pesa kadiri watakavyokuwa wakicheza na kuweza kubadili maisha yao.

Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Sadiki Elimsu akiipongeza Tigo kwa ubunifu wao wa kuanzisha mchezo huo utakao waneemesha wateja wao.

 

 

Lengo la mchezo huu ni kurejesha faida kwa wateja wetu wa Tigo Pesa ambapo mchezaji anaweza kujishindia mamilioni ya pesa kwa jinsi anavyoweza kushiriki.

Akielezea jinsia ya kushiriki mchezo huo Felician amesema unachotakiwa ni kupiga *150*01# kisha nenda 4 utaingia lipa bili hapo nenda namba 7 chagua mchezo, hapo nenda namba 2 ingia Dilipesa ambapo utakuta sehemu nne utakazotakiwa kuchagua sehemu ya kucheza.

Baadhi ya maofisa wa Tigo wakufuatilia uzinduzi huo.

Sehemu hizo ni Dodo ambayo mshiriki akibashiri kuanzia namba 0 mpaka 36 ukishinda unapewa pesa uliyoweka kama ni 1000 unapewa mara 36.

Sehemu ya pili ni Wapi Simba ambapo kuna maboksi matano ambapo ukishinda katika boksi moja unapewa kiashi ulichoweka mara nne.

Sehemu ya tatu ni Jack Pot Leo, ambapo ukiweka kuanzia shilingi mia tano unaweza kupata mamilioni kadili utakavyoweza kushiriki.

Na sehemu ya mwisho ni Soka Live hapa ukibashiri unaweza kujishindia kadiri unavyoweza kucheza alisema Felician kutoka Tigo.

Felician amewashauri watumiaji wa simu za mkononi kujiunga na mtandao wa Tigo ili waweze kutumia huduma za Tigo Pesa na kuweza kushiriki mchezo huo unaoweza kubadili maisha yao.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali akiwemo msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha Sadiki Elimsu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Sadiki ameipongeza Tigo kwa ubunifu wake wenye lengo la kuwanufaisha wateja wake.     HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave a Comment