
Zuchu buana ni msanii mtamu wa Bongo Fleva chini ya Lebo ya Wasafi iliyo chini ya Diamond Platnumz ambaye anasema kuwa mpenzi wake ni tajiri na amezama kabisa kwenye penzi lake.
Kauli ya Zuchu inakuja kufuatia moja ya shabiki kusema yeye siyo mzuri mara baada ya kuposti video akiwa na Lava Lava kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Na ubaya huo unaoniona nao naishi kwenye hekalu, nina gari mbili ya tatu nimeagiza yaja. A superstar ndiyo maana uko hapa una-comment, Bwana wangu ni tajiri na kakoleaje sasa, nasubiri vyako ndugu uliyenizidi uzuri,” anasema Zuchu ambaye kuna tetesi kwamba amemtunuku Diamond.
Tangu kutambulishwa kwa Zuchu ndani ya Wasafi Aprili, 2020 hajawahi kuweka wazi uhusiano wake licha kuwa na tetesi za hapa na pale ambazo mara zote amekuwa akizikanusha vikali.
STORI NA SIFAEL PAUL | GPL