×

Kocha Azam Atumia Dakika 90 Kuimaliza Yanga Azam Complex

Kocha Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin.

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Abdihamid Moallin, amesema dakika 90 alizotumia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya DTB inayoshiriki Championship, zimetosha kwake kuangalia upungufu wa kikosi chake kabla ya kukutana na Yanga.

 

Juzi Jumanne, Azam FC iliifunga DTB bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

 

Aprili 6, mwaka huu, Azam FC itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam.

Akizungumza na spoti Xtra, Moallin alisema: “Niliwaomba viongozi mchezo mmoja wa kirafiki baada ya kukaa muda mrefu bila ya kucheza mechi baada ya ligi kusimama kupisha mechi za Kalenda ya FIFA.

 

“Hivyo niliutumia mchezo huo kuangalia fitinesi za wachezaji wangu kwa ajili ya kuwaongezea wakati tukijiandaa kuwakabili Yanga.

 

“Nimeona upungufu kadhaa wa kikosi changu, hivyo nitafanyia kazi kwa siku hizi zilizobaki.”

STORI: WILBERT MOLANDI | SPOTI XTRA

SIMBA WAFUNGUKA KUMALIZANA NA ADEBAYOR, FEITOTO AIWAHI SIMBA LIGI KUU | KROSI DONGO

Leave a Comment