
TAARIFA zilizotolewa na kitua cha habari cha ELINT News zinadai kuwa ndege aina ya Mi-24 ambayo inasadikika kuwa chini ya wanajeshi wa Ukraine imelipua kituo cha hifadhi ya mafuta pamoja na ghala la silaha katika mji wa Belgorod nchini Urusi.
Jiji la Urusi lenye wakazi 369, 000 lipo maili 25 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine na maili 50 kutoka Kharkiv mashariki mwa Ukraine, Mapema wiki hii ziliibuka taarifa kuwa majeshi ya Ukraine yalivamia ghala la silaha lilopo Belgorod lakini baadaye ilionekana kuwa uvamizi huo haukutekelezwa na majeshi ya Ukraine bali ilikuwa ni makosa ya kibinadamu yaliyofanywa na watunza ghala nchini Urusi.