
MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Azam FC Shaaban Iddi Chilunda anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nne baada ya kupata majeraha ya goti katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Dtb.
Chilunda akiongoza na Daktari wa Timu Dkt Mwanandi Mwankemwa wameelekea Cape Town Afrika ya Kusini kwa ajili ya kufanya vipimo vya MRI kutokana na majeraha hayo.
Baada ya kufanyiwa vipimo hivyo amegundulika kupata madhara ya kuumia Mtulinga (Ligament) wa Kati-Pembeni, hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka Klabuni.

Daktari Robert Nicolas kutoka Hospitali ya Orthopaedic Surgeon Vicente Palloti ambaye anamfanyia uchunguzi amethibitisha kuwa Chilunda hana haja ya kufanyiwa upasuaji lakini anatakiwa kae nje ya Uwanja kwa takribani wiki nne baada ya hapo ataanza kufanya mazoezi mapesi na atakuwa amepona kabisa.