
KAMPUNI ya Mo Green International Company Limited inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo imezindua kiuatilifu cha kuuwa wadudu wanaoshambulia zao la pamba na magonjwa yanayoshambulia zao hilo kiitwacho Mo Strong ambacho kinatarajiwa kuwa mkombozi wa zao hilo.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari Mkurugenzi Mtendaji wa Mo Green International Limited, Matolo Patrick Kessy amesema lengo kuu la kuzindua kiuatilifu hicho kuongeza thamani katika zao la pamba ambalo limekuwa na changamoto nyingi kutokana na wadudu waharibifu pamoja na magonjwa yanayolishambulia zao hilo na kulifanya lisiwe na thamani hapa nchini. Mkurugenzi Matole alisema;

“Mo Green International Limited ni kampuni ya kitanzania ambayo inajihusisha na uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo hapa nchini.
“Lengo letu kubwa ni kushirikiana na wakulima kuhakikisha wanapata mafunzo sahihi katika kutumia viuatilifu na kulinda mazao yao ili wajiongezee kipato.

“Katika zao la pamba kuna changamoto nyingi sana zinazosababishwa na wadudu wa aina mbalimbali pamoja na magonjwa yanayolishambulia zao hilo.
“Kuna wadudu wanaokata au kutafuna zao hilo na kuna wanaofyonza ile pamba na kusababisha pamba yetu hata ikipelekwa sokoni ikutwe iko daraja la pili badala ya daraja la kwanza na hivyo mkulima kupata malipo pungufu kufikia alisilimia 70 mpaka 90 tofauti na mategemeo yake kupata kipato cha asilimia 100 kutokana na nguvu alizotumia.

“Hivyo basi katika kumlinda mkulima wa hapa nchini kampuni ya Mo Green International Limited imeleta kiuatilifu hiki kipya cha Mo Strong ambacho ni bingwa wa kudhibiti wadudu hao waharifu kama vile boronce, ambaye ni funza mwenye nywele ambaye kazi yake ni kukata zao la pamba.
“Mo Strong pia ni kiboko ya mdudu mwingine anayeitwa kangambili huyu ni chawa wa kijani pamoja na kuwaangamiza kuna vidomonzi wengine ambao kazi yao ni kushambulia na kuharibu kabisa zao la pamba.
“Awali kulikuwepo na dawa nyingi lakini huyu mdudu anayefyonza zao la pamba aliendelea kusumbua hivyo, Mo Green ilishirikiana na kituo cha utafiti cha Kilimo cha Ukiriguru kufanya utafiti kwa zaidi ya miaka mitatu na kuibaini Mo Strong kuwa ndiyo suluhisho la wadudu hao utafiti huo kupitishwa na taasisi ya viuatilifu ya TPRI.
“Kupitia kiuatilifu hiki sasa wakulima wa pamba wamepata mkombozi na kama mnavyojua hapa nchini kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu kama Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan ambavyo amekuwa akitusisiza siku zote kuongeza juhudi na kuwekeza kwenye sekta ya kilimo.
“Nimalizie kwa kuishukuru na kuendelea kuiomba serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na taasisi binafsi katika kuinua sekta ya kilimo,” alimaliza kusema Mkurugenzi Matolo.
Naye Afisa Kilimo wa MO Green International, Alex Michael amesema kiutilifu hicho kilichozinduliwa baada ya kufanyiwa utafiti wa zaidi ya miaka mitatu na kupitishwa na TPRI ndiyo suluhisho katika zao la pamba.
“Pamoja na zao la pamba kampuni yetu ina viutilifu vya kudhibiti wadudu wengine waharibifu wa mazao mbalimbali kama vile korosho na mengineyo.
“Tuna viuatilifu hivyo ni kama vile Movil, Mokalate, Mukron ambavyo ni kiboko kwenye zao za korosho pia tuna mabomba ya upuliziaji dawa za kuuwa wadudu hao yaitwayo Mo Power” alimaliza kusema afisa huyo. HABARI / PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL