×

Rais Samia Azindua Nembo Na Tarehe Ya Sensa Ya Watu Na Makazi Ya Mwaka 2022 Zanzibar (Picha +Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua rasmi Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika rasmi, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.

RAIS  wa Tanzaniza, Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi nembo ya sensa na kutangaza siku ya sensa ya watu na makazi itakuwa Jumanne Agosti 23, 2022.

 

RAIS  Samia amefanya uzinduzi wa nembo hiyo na kutangaza siku hiyo ya sensa leo Ijumaa Aprili 8, 2022 katika hoteli ya Golden Tulip mjini Unguja, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye kukata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo itaanza kutumika baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.

Rais Samia amesema shughuli ya uhesabuji watu inaisaidia Serikali kupanga vyema mipango yake ya maendeleo.

“Hili sio jambo geni kwa hiyo ni muhimu na tujitahidi kukamilisha mipango hii kwa manufaa ya Taifa letu,” amesema

 

Rais Samia ameagiza nembo hiyo itumike kwa shughuli zote za kiserikali na taasisi binafsi ili kuhamasisha wananchi waweze kutambua umuhimu wa kihesabiwa.

Rais Samia, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Sensa, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo rasmi wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itaanza kutumika, baada ya kutangaza kuwa Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar.

“Kwa taasisi za Serikali nembo hii iwekwe kwenye machapisho, website na mitandao ya kijamii lakini kwa upande wa taasisi binafsi zinaweza kuwekwa hata kwenye vifungashio au risiti na tiketi, kikubwa kila sehemu tuone hiyo nembo,” amesema Rais Samia

Awali Mwenyekiti wa kamati ya sensa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema siku ya sensa imepangwa kwa kuzingatia maombi ya viongozi wa dini isiwe siku ya ibada.

Rais Samia, akikabidhi Nembo ya vyeti maalum kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. John Jingu, kuashiria kumpa Jukumu la kuanza kazi hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Nembo ya Sensa ya Watu na Makazi ambapo Sensa hiyo itafanyika tarehe 23 Agosti 2022 nchi nzima. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo tarehe 08 April 2022 mjini Zanzibar. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dkt. Hessein Ali Mwinyi.

Majaliwa amesema mpaka sasa maandalizi ya shughuli hiyo ya sensa yamefikia asilimia 79 na kwamba kazi hiyo inaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya Serikali zote mbili; Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua nembo na tarehe ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Zanzibar leo tarehe 08 Aprili, 2022 Golden Tulip Hotel, Zanzibar.

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment