×

Meneja wa Mwamnyeto Afunguka, Adai Simba Wanamsumbua Mteja Wake

                       Beki wa kati na nahodha wa klabu ya Yanga Bakari Mwamnyeto

MENEJA wa Mchezaji wa Yanga Bakari Mwamnyeto aitwaye Kassa Mussa amedai Klabu ya Simba inamsumbua sana juu ya uwezekano wa kumsajili Mteja wake ambaye ni mchezaji na nahondha wa klabu ya Yanga Bakari Mwamnyeto.

 

Mussa amesema kuwa Simba wameweka mezani ofa kubwa mno ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na mbali na Simba Mwamnyeto amepata ofa nyingine Zaidi ya tatu kutoka mataifa ya Ugiriki na Malta.

 

“Simba wanasumbua sana nisiseme uongo, wamekuwa wakiibuka na ofa kubwa kubwa, ofa yao ni kubwa hasa ambayo nayo tumeamua kuichukua na kuendelea kuifanyia kazi.

          Nahodha wa klabu ya Yanga Bakari Mwamnyeto anayetakiwa na klabu ya Simba

.
“Ukiacha Simba, Bakari ana ofa nyingi sana, kuna ofa tatu au nne hivi, kuna klabu ya Ugiriki, Malta na nyingine moja bado tunazungumza nazo.” Alisema Meneja wa Bakari Nondo Mwamnyeto.

Leave a Comment