×

Urusi Yaanza Mashambulizi Mashariki Mwa Ukraine, Zelenskiy Afunguka

Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskiy.

Urusi hatimaye imeanza kufanya mashambulizi yaliyokuwa yamesubiriwa kwa muda mrefu mashariki mwa Ukraine. Haya yamesemwa na Rais wa Ukraine Volodomyr Zelenskiy kupitia ujumbe alioutoa kwa njia ya video.

 

Zelenskiy amethibitisha kwamba mashambulizi yameanza kufanywa katika eneo la Donbass. Wakati huo huo kiongozi huyo amethibitisha kwamba Ukraine itaendelea kupambana.

 

Kabla tangazo la Rais Zelenskiy, jeshi la Ukraine lilikuwa limetoa tamko kama hilo likisema kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya mabomu.

 

Katika siku za hivi karibuni, Urusi ilikuwa imeongeza idadi ya wanajeshi wake mashariki mwa Ukraine huku wanajeshi hao wakiondolewa katika sehemu zengine.

MIJADALA INAENDELEA BUNGENI, WABUNGE WANATOA HOJA KONKI, SPIKA TULIA ANAONGOZA KIKAO…

Leave a Comment