×

Marekani Yaamua Liwalo na Liwe, Yaipatia Ukraine Msaada wa Ndege za Kivita

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

RIPOTI kutoka Ukraine zinasema taifa hilo limepokea ndege za kivita kutoka Marekani kwa ajili ya kujilinda katika uvamizi unaofanywa na Urusi nchini humo.

 

Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani John Kirby, kwa sasa Ukraine ina ndege zaidi za kivita ikilinganishwa na wiki mbili zilizopita.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani John Kirby

Kirby lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na zilikotengenezwa ndege hizo au muundo wake. Rais wa Ukraine Volodomyr Zelensky alikuwa ameitaka NATO kutuma msaada wa ndege za kivita nchini humo.

 

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema nchi hiyo itaipa msaada wa silaha nzito za kijeshi Ukraine kufuatia wito wa msaada uliotolewa na Rais Zelensky.

Leave a Comment