×

Usiku wa Leo Kugeuka Kuwa Usiku wa Historia, ni Fury vs Whyte Kuzichapa

Tyson Fury dhidi ya Dillian Whyte kuzichapa usiku wa leokwenye pambano la uzito wa juu

USIKU wa leo, April 23, 2022 zitapigwa ngumi kali za uzito wa juu (heavy weight) kati ya miamba miwili, Tyson Fury na Dillian Whyte katika Ukumbi wa Wembley Stadium, London nchini Uingereza.

 

Pambano hilo la raundi 12 ni la kuwania mkanda wa World Boxing Council World Heavy Title ambalo limeandaliwa na mapromota Bob Arum kupitia kampuni yake ya Top Rank na Frank Warren kupitia Kampuni ya Queensberry Promotions.

Dillian White bondia wa uzito wa juu

Katika pambano la mwisho, Fury alimtwanga Deontay Wilder ‘Bronze Bomber’ kwa Knock Out huku Dillian Whyte naye akimtwanga Alexander Povetkin kwa KO.

 

Unadhani nani atakayemshikisha adabu mwenzake pale Wembley Stadium?

Leave a Comment