
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Spika wa Bunge, Tulia Ackson Familia, Wabunge na Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama aliyefariki dunia leo katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani.
“Natuma salamu za pole kwa Spika Mhe.@TuliaAckson Familia, Wabunge na Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Irene Ndyamkama aliyefariki dunia leo katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani. Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Samia.

