×

Rais Samia Ampongeza Rais wa Ufaransa kwa Kushinda Uchaguzi kwa Awamu ya Pili

Rais mteule wa Ufaransa Emmanuel Macrona anayeingia madarakani kwa awamu ya pili

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amempongeza rais wa Ufaransa Emmanuel Macron baada ya kushinda kwenye uchaguzi wa Rais nchini Ufaransa mapema jana.

 

Kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Rais Samia ameandika:

Mgombea mwenza kwenye kiti cha urasi wa Ufaransa Marine Le Pen aliyeshindwa

“Natoa pongezi kwa Mheshimiwa Emmanuel Macron pamoja na Chama chake kwa ushindi walioupata kwenye uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, nataka kukuhakikishia ushirikiano wa kutosha na nchi ya Tanzania ipo tayari kufanya kazi kwa ukaribu nan chi ya Ufaransa pamoja na watu wake ili kuhakikisha tunakuza shughuli zetu za kiuchumi na kijamii. Hongera sana!’

 

Macron amepata jumla ya 58% ya kura zote akimshinda Marine Le Pen na kuweka rekondi ya kuwa Rais wa kwanza ndani ya miaka 20 kurudi madarakani baada ya kukaa madarakani katika muongo wa kwanza.

 

 

Leave a Comment