×

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres Kukutana na Rais wa Urusi Putin leo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatazamiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow baadaye leo lakini matarajio kutoka kwa mkutano huo yanasemekana kuwa madogo baada ya juhudi kadhaa za kidiplomasia kushindwa kufikia sasa.

Mazungumzo kati ya Putin na Guterres yanatarajiwa kuangazia mji uliozingirwa wa Mariupol ambapo licha ya kutangaza ushindi, vikosi vya Urusi vimeshindwa kuchukua vyuma vya Azovstal.

Vikosi vya Ukraine vilisema mapema Jumanne kwamba Urusi iliendelea kuzuia vitengo vyake kwenye kiwanda hicho.Ukraine imemtaka Guterres kudhamini ukanda wa misaada ya kibinadamu ili kuwaondoa raia wanaohifadhiwa ndani ya Azovstal.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia anatarajiwa kusafiri kuelekea Kyiv siku ya Alhamisi ambapo atakutana na Rais Volodomyr Zelensky.

Marekani pia inatarajiwa kuanza mazungumzo ya ulinzi kuhusiana na Ukraine na mataifa kadhaa leo, huku waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akiwa mwenyeji nchini Ujerumani.

Mazungumzo haya yanakuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Moscow Sergei Lavrov ameonya hatari ya Vita vya Tatu vya Dunia “ni kubwa” na kukosoa mbinu ya Kyiv ya mazungumzo ya amani ya kuyumba.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, hata hivyo, alijibu kwamba Lavrov alikuwa akijaribu “kuitisha dunia” kutokana na kuunga mkono nchi hiyo.

Leave a Comment