
MAPEMA leo zimeibuka taarifa juu ya kifo cha moja kati ya mawakala maarufu wa wachezaji barani Ulaya Mino Raiola ambapo vyombo mbalimbali vya habari duniani vimeripoti kifo chake kabla ya kukanusha taarifa hizo.
Katika hali ambayo imewaacha na mshangao mkubwa mashabiki na wadau wa soka duniani kote ni kwamba Wakala huyo ambaye taarifa za kifo chake zimeenea duniani kote ametoa taarifa kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiandika:

“Hali ya sasa ya afya kwa mtu anayedhaniwa, ni kwa mara ya nne sasa ndani ya miezi kadhaa wameniua. Inaonekana pia naweza kuzinduka.”
Mino Raiola ni moja ya mawakala wakubwa ambaye anawasimamia wachezaji mastaa wakubwa duniani akiwemo Erling Haaland, Paul Pogba pamoja na Zlatan Ibrahimovic.