×

EU Yaibua Mpango wa Kuizuia Urusi Kuuza Mafuta Barani Ulaya na Dunia kwa Ujumla

Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen

UMOJA wa Ulaya umeibuka na mpango wa kuiwekea vikwazo vingine nchi ya Urusi kuhakikisha inapigwa marufuku kuuza mafuta barani Ulaya na Dunia kwa ujumla, lengo la kutekelezwa kwa mpango huu limepangwa kufikia mwishoni mwa mwaka 2022.

 

Hayo yamebainishwa na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen ambapo ameliambia Bunge la Ulaya kuwa sasa linaingia katika awamu ya sita ya vikwazo inayowekewa nchi ya Urusi kulenga uchumi wake lakini pia propaganda zake za kisiasa.

 

Akitoa maelezo mbele ya Bunge la Umoja wa Ulaya Ursula amedai Rais wa Urusi Vladimir Putin alitaka kuiondoa Ukraine kwenye ramani ya dunia lakini sasa nchi yake ndiyo itaangamia:

Urusi inatarajiwa kukumbwa na anguko kuu a uchumi endapo itafungiwa kuuza mafuta yake barani Ulaya na Dunia kwa ujumla

“Tutahakikisha tunaachana na mafuta ya Urusi katika mbinu sahihi, katika namna mabyo itaturuhusu sisi na washirika wetu kupata nishati mbadala na ya kutosha lakini katika muda huohuo tuwe makini kuwa tunapunguza ukali wa gharama katika soko la Dunia.” Alisema Ursula.

 

Ursula amebainisha kuwa mafuta ghafi yatakusanywa kwa kipindi cha miezi sita kisha yatachakatwa kufikia mwisho wa mwaka 2022, japo hakusita kubainisha changamoto itakazopitia nchi mbili ambazo zinategemea moja kwa moja mafuta ya Urusi, Slovakia na Hungary ambazo zenyewe zitapewa muda wa ziada kuhakikisha zinatafuta njia mbadala ya kupata nishati ya mafuta ya kutosha.

 

Rais huyo wa Umoja wa Ulaya amedai kuwa lengo kuu ni kuongeza presha kwa Urusi lakini ndani ya muda huohuo kuhakikisha wanapunguza gharama za mafuta sokoni kwa wasjirika wao duniani lakini pia kuhakikisha uchumi unabaki kuwa imara.

Moja ya Kampuni za mafuta zinazouza nishati hiyo barani Ulaya

Aliendelea kutoa maelezo ya kina ya namna ambavyo Umoja wa Ulaya unataka kuisaidia Ukraine kujijenga upya.

 

“Tunataka Ukraine ishinde vita hii, uchumi wa Ukraine ulitarajiwa kuporomoka kwa asilimia 35 hadi 50 ndani ya mwaka 2022 na itahitaji zaidi ya Euro Bilioni 5 kwa mwezi kuhakikisha nchi inahimili mapambano dhidi ya Urusi hivyo lazima tuchangie.”Alinukuliwa Ursula wakati akihutubia Bunge la Umoja wa Ulaya.

 

Mpango wa Umoja wa Jumuiya ya Ulaya (EU) ni kuhakikisha Urusi inakumbwa na vikwazo katika nyanga tatu muhimu ya kwanza ikiwa ni Nyanja ya kiuchumi kwa kuzuiliwa kuuza mafuta yao ndani ya Umoja wa Ulaya lakini pia Duniani kote, Nyanja ya pili ni kwenye majeshi ambapo EU imekuja na mpongo wa kuwafungulia keshi ya makosa ya uhalifu wa kivita maafisa wote wa jeshi waliohusika katika maangamizi kwenye mji wa Bucha na Mauripol na mpango wa tatu ni kuhakikisha inavifungia vituo vyote vya Televisheni ili kuzuia propaganda za Urusi kuhusu vita hiyo.

 

 

Leave a Comment