
VIKOSI vya majeshi ya Marekani, Uingereza, Latvia na Estonia vimefanya mazoezi ya pamoja Magharibi mwa nchi ya Finland.
Katibu Mkuu wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace ameongelea kuguswa na uwezekano wa Finland na Sweden kujiunga na Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi NATO.
Finland na Sweden siyo wanachama wa NATO na tangu Urusi ifanye uvamizi katika nchi ya Ukraine nchi hizo zimekuwa na nia ya kujiunga na NATO japo zimekuwa zikikumbwa na upinzani mkubwa pamoja na vitisho vya mashambulizi ya nyuklia kutoka kwa Urusi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa hakuna mtu anayeweza kutabiri kuwa Urusi haiwezi kuvamia nchi nyingine kutokana na ukiukwaji wake wa sheria za kimataifa baada ya kufanya uvamizi nchini Ukraine, na Ujerumani ipo tayari kuzisaidia nchi za Finland na Sweden kama zitaamua kujiunga na NATO.

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umevunja makubaliano ya maadhimio yaliyowekwa baada ya vita ya pili ya dunia jambo lililosababisha mataifa ya Ulaya kubadili mfumo na mbinu za ulinzi.