×

Supastaa wa Muziki Kutoka Nchini Guinea Grand P Ajimaliza kwa Mpenzi Wake

Msanii raia wa Guinea Grand P

MOUSSA Sandiana Kaba almaarufu Grand P; ni staa wa muziki na mitandaoni kutoka nchini Guinea ambaye amedhihirisha mahaba yake yote kwa mpenzi wake, Eudoxie Yao kwa kuchorwa tattoo ya jina lake mkononi.
Grand P amepiga hatua kubwa ya kuchorwa tattoo hiyo yenye maandishi; ‘Love Eudoxie’ kwenye kifundo cha mkono wake wa kushoto.

Grand P akiwa na mpenzi wake Eudoxie Yao

Eudoxie amefurahia kitendo hicho na kubainisha kuwa mapenzi ambayo mumewe anampa ni matamu mpaka baasi.
Haya yanajiri takriban miezi miwili tu baada ya Grand P kumvisha mrembo huyo pete ya uchumba.
Grand P mwenye maumbile ya kipekee alionekana akimuomba mpenzi wake wa muda mrefu wafunge ndoa katika mojawapo ya vituo vya televisheni nchini Guinea.

Eudoxie Yao alifurahia hatua hiyo na kusema kuwa ana kazi kubwa ya kufanya katika kuafikia maamuzi ambayo hatayajutia mbeleni.

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment